JUA MATUNDA 5 YANAYOWEZA KUKUPATIA MUONEKANO MZURI WA NGOZI YA MWILI WAKO


Baadhi ya watu wamekuwa wanachukulia  kirahisi ulaji wa matunda, lakini
unapaswa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu kwani yanatukinga
na magonjwa mbali mbali na pia hutengeneza muonekano mzuri wa ngozi ya
miili yetu.
 Kunakila sababu za kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu
kwa sababu huongeza vitamin kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule
matunda kila siku:

 AVOCAD Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa
juice, lakini huenda watu wakawa hawalipendi kwasababu ya kutokuwa na
sukari katika radha yake. Tunda hili linavitamini kibao, ambapo pia
huongeza mafuta mwilini, kwa wale walitumialo mara kwa mara.Unashauriwa
kula au kunywa juice ya avocado wakati wowote endapo kama huna matatizo
yoyote yanayohusiana na kuzidi kwa mafuta mwilini.Pia tunda hili
huongeza uzito endapo utalitumia mara kwa mara.

APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na
wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani
na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika
kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia
kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze
uhalisia wake.

NDIZI: Hili pia ni tunda lenyejina kubwa kwa watu wengi wanaojali
ulaji wa matunda, kwani nitamu na lenye ladha safi.Tunda hili husaidia
kulainisha ngozi ya uso iliyokauka, kwa mfano utakuta kuna baadhi ya
mafuta au losheni zimecholwa ndizi.Kula ndizi ili urekebishe ngozi ya
uso wako pamoja na kuupa uwezo mzuri wa  ukumeng'enya chakula.

PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta,
kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako.
Papai  pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na
enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka
kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na
papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha
utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa
siku mbili.

CHUNGWA: Hili ni chungwa maarufu sana linalosaidia kurudishia ngozi
iliyodhurika na kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia ni rahisi
sana, chukua juisi ya chungwa ya baridi kisha paka usoni, acha kwa
dakika 10 kisha osha utaona matokeo yake

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard