Tazama Ndugu wa Babu Seya Walivyofurika Gerezani Baada ya Kusikia Wamepewa Msamaha


BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoa msamaha kwa familia ya Nguza Viking aliyekuwa amehukumiwa na mwanaye Papii Kocha kifungo cha maisha, ndugu wa familia hiyo na marafiki wamefurika nje ya Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kumshukuru Rais.

Baadhi ya marafiki wa familia ya Babu Seya wakimpongeza Mbangu.
 Mtandao huu umenasa baadhi ya picha zinazoonesha tukio zima eneo hilo hadi kuachiwa wanamuziki hao maarufu ambao tayari wameingia uraiani.

Mtoto wa Babu Seya, Mbangu Nguza (katikati) naye akiwa nje ya gereza hilo.
 “Tunamshukuru Mungu, tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuwasamehe ndugu zetu. Mungu ambariki,” alisema Mbangu, mtoto wa Babu Seya.

 Babu Seya na  Papii wameachiwa leo baada ya kutumikia kifungo hicho kwa takriban miaka 13 katika Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru zilizofanyika mkoani Dodoma hii leo.

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard