MCH LUSEKELO AWAKANDIA WANAHABARI KWA KUREPORT TUKIO LAKE LA KULEWA NA KUFANYA FUJO

Yatosha

Siku tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo akisema anaishi kana kwamba hana jirani.

“…Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.Lusekelo amesema Yesu ambaye ni  mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake.Amesema magazeti hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpasha ila Mungu pekee.

Katika mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.lusekelo

Alhamisi iliyopita, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani yake lakini mchungaji huyo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo ambalo lilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia mzozo huo, kuandika kwa kirefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Picha ya video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha mtu anayedaiwa kuwa ni mchungaji Lusekelo akijibizana na sauti ya mwanamke, ambaye haonekani, huku gari la rangi nyeusi aina ya Toyota Landcruiser likiwa limeegeshwa katikati ya barabara ya mtaani na kuzuia mengine kupita.

“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti yasiandike habari hizo?”

“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani, matatani babu yako.”

“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa mmemaliza,”amesema.

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard