? JUAN MATA VS OSCAR: NANI ANASTAHILI KUCHEZA KAMA NAMBA 10 NDANI YA CHELSEA?


Jose Mourinho ameweka wazi kabisa kwamba Oscar ndiye mchezaji anayempa kipaumbele cha kwanza katika jukumu la kucheza kama mshambuliaji wa pili ndani ya kikosi chake. Juan Mata, ambaye kwa miaka miwili iliyopita amekuwa mchezaji bora wa Chelsea chini ya makocha tofauti hivi sasa anahangaika kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho. Jambo ambali limekuwa gumu kwa watu wengi kuelewa ukiangalia mchango wake ndani ya timu tangua alipohamia timu hiyo akitokea Valencia msimu wa 2011-12.

Nini Mourinho anachokitaka kutoka kwa mchezaji anayecheza namba 10?
Jose Mourinho anahitaji mchezaji ambaye atajituma kucheza kwenye nafasi hiyo huku akirudi nyuma katika safu ya kiungo cha juu ili kuisadia timu inapokuwa haina mpira. Oscar ni mchezaji anayeweza kucheza kwa namna hiyo, kitu ambacho ni kigumu kwa  Juan Mata kukifanya.

Dhidi ya Fulham kwa mfano, Oscar aliweza kufanya tackling nyingi kuliko mchezaji yoyote wa Chelsea, tackles sita, namba kubwa kwa mchezaji anayeshambulia. 
tackles
Pia ni vizuri kuangalia ni wapi aliweza kufanya tackles hizo, tano kati ya hizo zilikuwa katika nusu ya uwanja upande wa Fulham, hii inaonyesha kwamba Oscar alikuwa anawalazimisha Fulham kucheza kwao zaidi kwa kujaribu kuchukua mipira na kuisaida Chelsea katika mashambulizi. Ni vigumu kufikiria kama Mata angeweza kufanya hivi na kupatia kama Oscar. Hiki ni kitu ambacho Mourinho amekizungumzia akisema anataka timu yake kwa kujihami mapema kabla ya kutokea kwa madhara kwa kujaribu kupora mipira kwenye nusu ya uwanja ya adui. Kitu ambacho akicheza kama namba 10 Oscar anakipatia sana kama tulivyoona kwenye picha hapo juu. 

Mata yupo tofauti kiasi, akiwa mzuri zaidi katika kushambulia kuliko kuwa na kasi na tayari kupambana kwa nguvu kupora mipira kama Oscar.  Mata anapendelea kucheza nyuma ya mshambuliaji kuliko kurudi kwenye maeneo ya nyuma wakati timu inapokuwa haina mpira. Pindi Mata anaporudi nyuma huwa anarudi kuchukua mipira kutoka wachezaji wa nyuma, na sio kwenda kujaribu kupora mpira.

Mourinho amesema kwamba Oscar anaweza kukimbia na mpira, kutanua uwanja na kutengeneza nafasi, mambo yanayomuongezea sifa za kuwa namba 10 sahihi kabisa kwa mbinu za kiufundi cha Mourinho. Mpaka kufikia hapo ni wazi Oscar ataendelea kuwa kipaumbele cha kwanza cha Mournho linapokuja suala la namba 10. 

Hatma ya Juan Mata
Jose Mourinho pia amekaririwa akisema anataka kuona Mata na Oscar wakianza pamoja, jambo ambalo linawezekana. Mourinho angeweza kumtumia Mata kama winga wa kulia na Oscar kama namba 10. Anachotaka Mou ni Mata kucheza nje kidogo ya upande wa kulia, akiingia ndani na pia kurudi nyuma muda wote kumsaidia mlinzi wa kulia. Hiki si kitu ambacho Mata anaweza kukileta ndani ya timu kiurahisi isipokuwa tu pale atakapojitahidi kuweza kujituma katika kukaba, kitu ambacho hajazoea. Ikiwa Mourinho atafanikiwa kupata kilicho bora kwa mahitaji yake kutoka kwa wachezaji hawa wote wawili then labda Chelsea inaweza kupata mwanga mzuri zaidi. 

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard