Mambo ya Kishamba Ambayo Mwanaume wa Sasa Hutakiwi Kuyafanya



1. Kufuata mkumbo, kutokuwa na maamuzi yako mwenyewe.

2. Kuongea lugha chafu, huwezi kumaliza sentensi bila matusi.

3. Kuvaa mlegezo.

4. Kunyoa panki, kiduku au kuacha afro.

5. Kuvaa viatu vya four angles au vyenye soli kubwa.

6. Kukimbia mimba au kutelekeza familia.

7. Kunywa pombe bila kipimo, kushinda bar bila sababu maalumu utadhani wewe kreti.

8. Kuvaa suruali za model au bwanga au kuvaa mayeno.

9. Kumpiga mwanamke awe mkeo, mpenzi wako au hata rafiki tu.

10. Kuwa na hulka ya kupigana, yani huwezi ku-solve tatizo kwa njia nyingine zaidi ya kuwaza kupigana.

11. Kuwa wa kwanza kulala na wa mwisho kuamka.

12. Kuvaa tshirts zenye maneno makubwa na mbaya zaidi yasiyo na maana.

13. Kulakula hovyo, hyo tabia tuwaachie wanawake

14. Kuvaa vitu oversize ili udumu nayo muda mrefu.

15. Kuvaa mikanda oversize, unakuta mkanda mkubwa had uajikunja ukiwa kwenye luks au una buckle kubwa.

16. Kuvaa tshirts zilizokatwa mikono.

17. Kuvaa boshori.

18. Kukaa vijiweni bila kuwa na shughuli ya maana kufanya.

19. Kuwaza starehe muda wote, weekend ikifika utasikia 'mwana bata wapi?'

20. Kuhonga vimada huku wanao hawana viatu au uniform za shule zimechakaa kupitiliza!! Na mbaya zaidi unawalaza hadi njaa we unakula raha na vimada tu by Ligogoma

21. Kuendekeza michepuko ilhali umeoa tena mke mrembo kweli kweli by Ligogoma

22. Kutojiwekea malengo ya kiuchumi, unaishi tu kama ndege.

23. Kuacha mindevu hovyohovyo bila maana.

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard