MWANAMUZIKI mwenye
vituko kila kukicha Bongo, Baby Joseph Madaha, ametoa dukuduku lake la
moyoni na kusema kuwa kila kukicha anayatamani mapenzi ya Wema Sepetu
na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kama angekuwa yeye.
Akizungumza
na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na Diamond
anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na kuhamasisha
kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua ya kuwaonea
wivu.
“Kiukweli
nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati natamani niwe
mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa Bongo kama hii
jamani, naitamani hadi basi,” alisema Baby.
No comments:
Post a Comment