Kauli ya Mtoto wa Babu Seya Baada ya Familia Yake Kuachiwa Huru



IKIWA ni saa chache baada ya Mwanamuziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu  Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais Magufuli, mtoto wa mwanamuziki huyo, Michael Nguza amesema anamshukuru Mungu kwani familia yao ipo huru kuanzia leo.

Michael Nguza ambaye kwa sasa anajiita Nabii Michael baada ya kutoka jela amesema kwenye kesi hiyo aliyokuwa na ndugu zake:
“Namshukuru Mungu, Mungu ni mwaminifu. Siwezi kuongea mengi kwa sasa, nitatoa taarifa rasmi baadaye. Tunatarajia kufanya kikao cha familia ili kujadili suala hili na baadaye tutaulezea umma baada ya majadiliano hayo ya familia, naomba kuweni wavumilivu na wenye subira,” amesema Nabii Michael.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi wa kuachiwa huru kwa familia ya Nguza Viking, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa Mjini Dodoma wakati wa akihutubia  maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa mjini Dodoma wakati wa akihutubia  maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika. 

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard