TAMBWE AMIS, NA MABAO MENGINE 78 KATIKA MICHEZO KATIKA MECHI 35, - STEPHEN KESHI KUCHUKUA MIKOBA YA STEWART HALL AZAM??


Na Baraka Mbolembole 
Uliona namna Yanga ilivyouliwa na Azam FC? Uliona mabao ya kuvutia katika mchezo wa Simba na Mbeya City? Umesikia matokeo ya timu ya Rhino Rangers? Umemuona Hamis Tambwe? Na vipi kuhusu kipaji cha ufungaji cha Didier Kavumbagu? Tunahitaji nini zaidi ya mbinu za makocha na uaminifu wa wachezaji na viongozi kwa makocha wao?

Mabao manne yaliyofungwa na mshambuliaji, Hamis Tambwe yanaweza kuwa ' topiki' baada ya kupita miaka miwili pasipo kufungwa kwa ' hat-trick' katika ligi kuu Tanzania Bara, raia huyo wa Burundi alifunga wakati timu yake ya Simba, ikiifunga timu ya Mgambo JKT, mabao 6-0 na akafunga tena mara mbili katika sare ya 2-2 siku ya jumamosi

Raundi ya tano ya ligi kuu ilimalizika wikiendi iliyopita, na kutoa mabao 18 katika michezo 35 ambayo imeshapigwa hadi sasa. Mechi baina ya Azam FC na Yanga, ndiyo Iiyotoa mabao mengi zaidi ( matano) katika mechi za raundi hiyo, ambayo ilishuhudia pia vinara Simba SC wakivutwa shati katika uwanja wa Taifa na Mbeya City, sarte iliyozalisha mabao manne ya ‘ video’ kutoka kwa washambuliaji Hamis Tambe ( Simba), Paul Nongwa na Richard Peter ( City).

Ligi imekuwa ngumu kweli kweli, na uwepo wa udhamini wa ziada ya AZAM TV, na fursa ya kujiongezea wadhamini kwa kadri timu zinavyoweza kuwashawishi wawekezaji, kumeendelea kutoa mwanga kidogo kuwa huenda msimu huu ukawa ni moja ya misimu bora kwa baadhi ya timu nap engine kutoa ‘ bingwa wa ukweli’. Sijui ni kitu gani kitakachotokea upande wa Yanga endapo watajikuta katika wakati mgumu tena siku ya jumatano hii watakapocheza na Ruvu Shootings katika mchezo wa raundi ya sita, kama watapoteza kwa mara nyingine pointi itakuwa ni jambo zuri kwa Shootings, ambayo imekuwa ni moja kati ya timu zenye safu nzuri ya ulinzi.

KIMWAGA AMUOKOA KOCHA STEWART HALL 
Kinda wa Azam, Joseph Kamwaga aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Brian Omony aliweza kuchomoza katika soka la Tanzania baada ya kutumia vizuri pasi aliyopewa kwa mtindo wa ‘ counter attack’’ na kisha kuwapita walinzi, Kelvin Yondan na Mbuyu Twite na kuwapa ushindi wa kwanza timu yake katika michezo mitano iliyopita.
 Kabla ya mchezo huo, wachezaji wa Azam waliahidi mbele ya uongozi wao wa juu kuwa wataifunga Yanga, lakini kocha Stewart Hall ambaye alitoa machozi baada ya kumalizika kwa mchezo huo anaweza kuitwa ‘shujaa aliyekuwa ametengwa’. Baadhi ya wachezaji muhimu wa Azam waliondolewa katika kikosi cha kwanza na wapo ambao hawakujumuishwa kabisa katika mchezo huo. 
Na yote hiyo ilikuja baada ya Stewart kuhisi hawapo tayari kutetea kibarua chake kwa kuisadia timu kupata ushindi. Habari ambazo nimezipata ni kwamba Stewart, ‘hawivi chungu kimoja’ na baadhi ya viongozi wa juu wa klabu. Hivyo anaandaliwa matokeo ya kufukuzwa, wakati Nigeria itakapokuwa ikicheza na Ethiopia katika michezo ya kuzufu kwa fainali za kombe la dunia, baadae mwezi ujao na kufuzu pengine ndiyo Stewart atatulia, ila endapo Nigeria itatolewa basi hatakuwa na kibarua. Azam si wana pesa bwanaa., Stephen Keshi alikuwa atue klabuni hapo mara baada ya Boris Bunjak kutimuliwa oktoba mwaka jana, akatoa masharti ya kuja na msaidizi wake, Azam wakamwambia atasaidiana na Kally Ongalla, dili likafa na Keshi akatwaa taji la mataifa ya Afrika, mapema mwaka huu akiwa kocha wa Nigeria.

Azam wanahisi tayari wanahitaji kitu kikubwa zaidi ya nafasi wanayoipata, kumaliza nafasi ya pili mara mbili mfululizo, kumaliza nafasi ya tatu mara mbili mfululizo, baada ya kunusurika kushuka daraja katika msimu wao wa kwanza, Azam wanajiona wapo tayari kuwa mabingwa wa ligi kuu mbele ya timu za Simba na Yanga. Wakati mwingine pesa inaweza kununua kila kitu, lakini ushindi wa mataji hauji kirahisi. Ni kweli baada ya misimu sita tangu Azam ianzishwe wanastahili kutwaa ubingwa mbele ya Simba au Yanga?. Wapo katika mwendo mzuri na navyofahamu mimi lengo la awali la mmiliki ni baada ya miaka kumi ya kujijenga ndiyo wanaweza kutwaa ubingwa. Lakini wanataka kusimamisha saa, ila wanasahau kuwa muda hausimami daima.

Tayari timu hiyo imenolewa na makocha, Neidor Dos Santos, Itamor Amourin, Bunjak, na sasa Stewart achana na wale wazawa kama Habib Kondo, Silvester Marshi, huku Stewart aliondolewa na kurudishwa tena baadae. Ni idadi kubwa sana ya makocha kwa timu kama Azam, ndani ya miaka sita kuwa na mipango ya makocha wengi hivyo bila shaka kuna lengo la ziada ambalo Azam wanalo na si lile la kujiimarisha kwanza huku wakitoa changamoto ya kuwania mataji na Simba na Yanga, na kama ikitokea kutwaa ubingwa hilo liwe jambo lisilotarajiwa. Pesa wanayo, na pengine ndiyo sababu ya yote hayo, kutokea, pengine wanaweza kuwa tayari wamewatumia zaidi ya wachezaji 40- 50 wa kigeni tangu kuanzishwa kwake na hakuna aliyemaliza mkataba wake zaidi ya Ibrahim Shikanda ambaye amekuwa mmoja wa makocha wasaidizi klabuni hapo kwa sasa. 

Ila bado wachezaji Fulani Fulani wa Kitanzania wamebaki kuwa muhimu zaidi, ukichunguza wachezaji kama John Bocco, Salum Abubakary, Himid Mao, Wazir Salum, kipa Aishi Mwinula, wamekuwa wakifanya vizuri muda wote ni msingi wa timu yao na pengine ni kutokana na uaminifu wa vijana hao kwa walimu wao waliopita na waliyenaye sasa umekuwa ukiwapatia mafanikio, na, kuisadia timu yao.

Kwa soka la Tanzania hata kama mchezaji ataanza kucheza ligi kuu ya Tanzania akiwa na miaka 17 baada ya misimu mitatu anaitwa ‘ Mzee’, Salum anacheza msimu wake wa sita wa ligi kuu akiwa katika kikosi cha kwanza cha Azam, Himid baada ya kumaliza masomo mwaka uliopita naye amejikita katika kikosi cha kwanza kwa sasa, Bocco ‘hagusiki’ kikosini mwao, na wakati nyota hawa wakikua kiumri na kimchezo, wakiimarika kimbinu na kiufundi baada ya kupata bahati ya kufundishwa na walimu wa kigeni tangu wakiwa yosso, Azam wenyewe waaingia katika mipango ya kuivuruga timu. Kuna kundi makundi, kwa muda sasa wachezaji wamekuwa wakimkubali Stewart, na uongozi umekuwa ukimuona Muingereza huyo si mtu wa kuwafikisha wanakotaka kufika.

Chozi la Stewart katika uwanja wa Taifa baada ya kinda, Kimagwa kufunga bao la kushtukiza, lilikuwa na maana kwamba kuna wachezaji wamemsaliti, ni kwa mtazamo wangu zaidi lakini naweza kuwa sahihi na wengine pia. Kuna wachezaji wameingia katika ‘ mkumbo’ wa baadhi ya viongozi kwa kumsariti Stewart ili timu ifungwe, kisha afukuzwe. Nao wanaoneka kukubali hilo kwa kuwa keshi ndiye anaweza kuwa mbvadala wa Stewart. Sijui kwa nini ila wakati, ligi kuu yetu ikizalisha soka safi, timu zenye ushindani, makocha wenye mbinu nzuri, pengine tunahitaji udhamini wa lazima, ‘Uaminifu katika kila idara ndani ya klabu’ Bado tunahitaji kuona Simba na Yanga zikifungwa, Simba na Yanga zikiruhusu mabao ya kulazimishwa, tunahitaji kuona zaidi uwepo wa timu katika kujilinda na kushambulia, kuona ‘hat- trick’ zaidi kutoka kwa Tambwe, na kuona Yanga wakishika tena katika eneo lao na timu pinzani kupewa penati. Mohammed Kampira,

Hemed Morocco, Mbwana Makatta, Juma Mwambusi, Jackson Mayanja, Mecky Mexime, Charles Mkwasa, Jumanne Chale, na wengineo TUKIWATEGEMEA kutuletea nyota wengine wapya katika soka la Tanzania. Nasikia Yusuph Manji, aliocheza kale ka mchezo ketu….. Aaah, eti Manji alebeti Yanga inafungwa…. Yanga wakifungwa mji unatulia, kama United tu, wapenzi wa soka Dar walikuwa na wikendi mbovu. Liverpool, Simba, Yanga , Manchester United waliharibu . Mechi, 35, Mabao 78, Tamwe kinara wa mabao, tayari tunayo ‘ hat’ trick’, mabeki fungeni viatu. 0714 08 43 08

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard