Jose
Mourinho ameweka wazi kabisa kwamba Oscar ndiye mchezaji anayempa
kipaumbele cha kwanza katika jukumu la kucheza kama mshambuliaji wa pili
ndani ya kikosi chake. Juan Mata, ambaye kwa miaka miwili iliyopita
amekuwa mchezaji bora wa Chelsea chini ya makocha tofauti hivi sasa
anahangaika kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho.
Jambo ambali limekuwa gumu kwa watu wengi kuelewa ukiangalia mchango
wake ndani ya timu tangua alipohamia timu hiyo akitokea Valencia msimu
wa 2011-12.
Nini Mourinho anachokitaka kutoka kwa mchezaji anayecheza namba 10?
Jose
Mourinho anahitaji mchezaji ambaye atajituma kucheza kwenye nafasi hiyo
huku akirudi nyuma katika safu ya kiungo cha juu ili kuisadia timu
inapokuwa haina mpira. Oscar ni mchezaji anayeweza kucheza kwa namna
hiyo, kitu ambacho ni kigumu kwa Juan Mata kukifanya.
Dhidi
ya Fulham kwa mfano, Oscar aliweza kufanya tackling nyingi kuliko
mchezaji yoyote wa Chelsea, tackles sita, namba kubwa kwa mchezaji
anayeshambulia.
Pia
ni vizuri kuangalia ni wapi aliweza kufanya tackles hizo, tano kati ya
hizo zilikuwa katika nusu ya uwanja upande wa Fulham, hii inaonyesha
kwamba Oscar alikuwa anawalazimisha Fulham kucheza kwao zaidi kwa
kujaribu kuchukua mipira na kuisaida Chelsea katika mashambulizi. Ni
vigumu kufikiria kama Mata angeweza kufanya hivi
na kupatia kama Oscar. Hiki ni kitu ambacho Mourinho amekizungumzia
akisema anataka timu yake kwa kujihami mapema kabla ya kutokea kwa
madhara kwa kujaribu kupora mipira kwenye nusu ya uwanja ya adui. Kitu
ambacho akicheza kama namba 10 Oscar anakipatia sana kama tulivyoona
kwenye picha hapo juu.
Mata
yupo tofauti kiasi, akiwa mzuri zaidi katika kushambulia kuliko kuwa na
kasi na tayari kupambana kwa nguvu kupora mipira kama Oscar. Mata
anapendelea kucheza nyuma ya mshambuliaji kuliko kurudi kwenye maeneo ya
nyuma wakati timu inapokuwa haina mpira. Pindi Mata anaporudi nyuma
huwa anarudi kuchukua mipira kutoka wachezaji wa nyuma, na sio kwenda
kujaribu kupora mpira.
Mourinho
amesema kwamba Oscar anaweza kukimbia na mpira, kutanua uwanja na
kutengeneza nafasi, mambo yanayomuongezea sifa za kuwa namba 10 sahihi
kabisa kwa mbinu za kiufundi cha Mourinho. Mpaka kufikia hapo ni wazi
Oscar ataendelea kuwa kipaumbele cha kwanza cha Mournho linapokuja suala
la namba 10.
Hatma ya Juan Mata
Jose
Mourinho pia amekaririwa akisema anataka kuona Mata na Oscar wakianza
pamoja, jambo ambalo linawezekana. Mourinho angeweza kumtumia Mata kama
winga wa kulia na Oscar kama namba 10. Anachotaka Mou ni Mata kucheza
nje kidogo ya upande wa kulia, akiingia ndani na pia kurudi nyuma muda
wote kumsaidia mlinzi wa kulia. Hiki si kitu ambacho Mata anaweza
kukileta ndani ya timu kiurahisi isipokuwa tu pale atakapojitahidi
kuweza kujituma katika kukaba, kitu ambacho hajazoea. Ikiwa Mourinho
atafanikiwa kupata kilicho bora kwa mahitaji yake kutoka kwa wachezaji
hawa wote wawili then labda Chelsea inaweza kupata mwanga mzuri zaidi.
No comments:
Post a Comment