Mamlaka
nchini Nigeria zimesema kuwa hakukuwa na ulinzi katika chuo cha Kilimo
ambako wanafunzi 50 waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa wamelala.
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya tukio hilo lililotekelezwa na
wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wenye itikadi kali ya Kiislam wa kundi la
Boko Haram katika chuo hicho katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki
mwa nchi hiyo.
Ofisa mmoja wa serikali amesema, serikali na
jeshi la wataimarisha ulinzi kwenye maeneo ya shule na kuongeza kuwa
licha ya shambulio hilo masomo yataendelea kama kawaida
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment