MAJAMBAZI YATEKA BASI LA ABIRIA NA KUPORA SIMU NA FEDHA..

    Abiria hamsini na moja waliokuwa wakisafiri na basi la Taqwa kutoka  Bujumbura kuelekea Dar-es-Salaam wametekwa katika kijiji cha Milade wilayani Mkalama na kuporwa mali , simu na fedha zaidi ya shilingi milioni mia mbili hamsini.
Akieleza kamanda wa polisi mkoani Singida bwana Godfrey Kamwela  amesema watekaji hao waliwaamrisha abiria kushuka chini ya basi baada ya kuvunja vyoo na kuanza kuwasachi na kufanikiwa kupora simu, fedha za  kitanzania shilingi milioni tano ,dola za kimaerekani dola laki moja elfu sitini na  faranga zenye thamani ya elfu ishirini kufuatia tukio hilo kamanda Kamwela amewaomba wananchi na makampuni ya simu kushirikiana na jeshi la polisi ili kuweza kuwa kamata watu ambao wamefanya tukio hilo.

Kwa upande wake dereva la basi hilo bwana Ahamed Seif amesema gafla aliona majani barabarani na alipoangalia vizuri aliona kuna mawe makubwa  mawili  yakiwa barabarani na kushindwa  kuyakwepa ,baada ya kugonga mawe hayo magurudumu yote mawili ya mbele yalipasuka na gari  ikaserereka umbali wa mita mia moja.

Kwa upande wao abiria na majeruhi wamesema waliona gari likipoteza mwelekeo na baadaye walisikia sauti za watu zikiwaambia washuke na watoe fedha na simu zao,lakini abiria wengine wametupia lawama kwa wafanyakazi wa basi hilo kuchukuwa abiria wa njiani wakati basi likiwa limejaa na abiria hao inasadikiwa ndio waliokuwa wakiwasiliana mara kwa mara na watekaji.

Naye mganga wa wodi ya majeruhi ya hospitali ya mkoa wa Singida Dkt Banuba Deogratias amesema walipokea majeruhi  kumi na tisa walikuwa na mipasuko na majeraa ya kupigwa na fimbo, wameweza kuwatibu na kuruhusiwa isipo kuwa wengi wao hawana fedha  kwa sababu ni raia kutoka nchi za Burundi na Kongo walikuwa wakisubiri kukabidhiwa  kwa idara ya ustawi wa jamii ili wasaidiwe nauli za kurudi makwao.

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard