MUME HAKUWA MHUNI!
Akizungumza na Amani kwa majonzi mazito hivi karibuni, mjane wa marehemu aitwaye Salma Abdallah ambaye ni Muuguzi Mwandamizi wa Hospitali ya Chadibwa, Ukonga Ilala jijini Dar es Salaam alisema mumewe hakuwa na tabia ya uhuni na siku ya tukio ilikuwa mara ya kwanza kukutana na mwanamke huyo.
CHANZO CHA KIFO
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, ripoti iliyotolewa na daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambaye ndiye aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, ilionesha kuwa Hamad alitumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ‘viagra’ ndiyo maana mauti yalimkuta ghafla.
“Mume wangu alipata ajali mbaya mwanzoni mwa mwaka huu, akapata tatizo la presha na nguvu za kiume kupungua.
“Hivyo kwa mujibu wa ripoti ya daktari mtu ambaye ana presha akitumia dawa za kuongeza nguvu za kiume, hasa viagra uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa. Ripoti ilisema presha ilimpanda mume wangu wakati wa tendo akafa.
MWANAMKE ALIYEKUWA NA MAREHEMU AACHIKA
Kwa mujibu wa mjane huyo, mwanamke aliyekuwa gesti na mumewe siku ya tukio, Latifa aliachika kwa mumewe baada ya kutokea kwa tukio hilo kwani mume wake alimweleza hataki kumuona nyumbani kwake, kwa sasa anaishi kwa baba yake Majoe jijini Dar.
ILIKUWA SIKUKUU YA IDD EL FITR
Hamad alifikwa na mauti siku ya Idd Pili akiwa katika gesti moja iliyopo Kiwalani, Dar es Salaam ambapo alikuwa na mwanamke huyo.
Mazishi ya Hamad yalifanyika katika Makaburi ya Temeke, Dar huku ndugu wa marehemu wakimfutia kesi mwanamke huyo wakisema wanamwachia Mungu.
No comments:
Post a Comment