Wengi
tulidhani hili swala limeisha hasa baada ya wahusika wote kuzungumza
akiwemo mlalamikaji Dayna Nyange, producer Sheddy Clever wa Burn Records
aliyeitengeneza beat hiyo iliyoleta mzozo, na Diamond Platnumz
aliyeitumia beat hiyo katika single yake mpya ambayo ni talk of the town
‘My Number One’.
Sheddy
Clever ameongea exclusive na Bongo5 na kusema kuwa pamoja na kuwa yeye
ndiye producer na mmiliki wa beat hiyo iliyozua utata lakini Dayna
amemshitaki COSOTA kwa kumuibia beat aliyotumia Diamond katika ‘My
Number One’.
Sheddy
amesema alipokea simu kutoka COSOTA na kupewa taarifa kuwa anahitajika
kufika katika ofisi zao Jumatano hii (September 25) kwaajili ya kesi
hiyo.
Haya ndio maelezo ya Sheddy Clever:
“Juzi
ilikuwa tarehe 14 nimepigiwa simu na namba ngeni ambayo siijui
wakajitambulisha wao ni COSOTA, nikaambiwa nabarua yangu pale njiifuate
inipe muongozo kwamba nahitajika pale. Basi sikuwa nashaka wala na hofu
yoyote kwasababu mi ni mtu ambaye nafanya kazi na COSOTA ni watu ambao
wapo kwaajili ya kazi yangu ya muziki.
Kwahiyo
nikaenda nimefata hiyo barua kuja kufungua ile barua ni kuhusu mambo ya
Dayna. Dayna ameenda ameshtaki amesema kwamba ile beat ameibiwa kwahiyo
mpaka dakika hii mi sielewi kwamba ana matatizo gani huyo dada anasema
kwamba ile beat kaibiwa na je, unajua kwamba ni makosa kumuita mtu mwizi
kwahiyo anaweza kufunguliwa mashtaka kwanini amuite mtu mwizi, je
anauhakika gani au ushahidi gani ile beat kaibiwa.
Kwahiyo
nimeambiwa niende tarehe 25 ili niende nikaskilize inakuwaje, kwahiyo
mi ntaenda kuskiliza tarehe 25 tujue inakuwaje ili tuweze kupata muafaka
wa hili swala sababu mi sipendi haya matatizo….kwasababu naona yeye
anataka liwe tatizo kwasababu mi naona limeisha…mi nahisi linaendelea
kuwa kubwa zaidi, kwahiyo kama yeye anahitaji liwe kubwa basi litakuwa
kubwa zaidi kama anahitaji yaishe basi yaishe”.
Sheddy
aliongeza kuwa toka Dayna aanze kulalamika kupitia mitandao hajawai
kumtafuta hata mara moja ili angalau amuulize chochote, zaidi ya kusoma
habari zote katika vyombo vya habari na mpaka alipokuja kupokea barua ya
kuitwa COSOTA.
Sheddy
amesema katika barua hiyo wameitwa yeye, Diamond Platnumz pamoja na
meneja wa studio ya Burn Records aitwaye D.Manyuti. Hata hivyo Sheddy
aliongeza kuwa Diamond amesema hatahudhuria.
Mpaka
habari hii inaenda hewani nimejaribu kumtafuta Dayna Nyange ili
kuthibitisha kama ni kweli alifikisha malalamiko yake COSOTA kuhusu
swala hilo lakini simu yake haikupokelewa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment