NIMEVUNJA UCHUMBA WA MFANYAKAZI MWENZANGU KUMUOKOA RAFIKI YANGU..SIJUTII

                Ndugu zanguni akina dada,kaka akina baba na akina mama na wote mlio kwenye ndoa maandiko yanasema ndoa na iheshimiwe na watu wote tena wote, in short nimemuumiza dada mfanyakazi mwenzangu lakini sijutii hata kidogo.Ni kwamba dada ameanza kazi kama mwaka mmoja uliopita akatukuta sisi wakongwe tumetulizana ndani ya ofisi.Kutwa huyo dada ni kumzoea kila mwanaume ndani ya kampuni nzima anajifanya eti social wewe chezea Dar.

Baisi bi dada watu wakaanza kumfukuzia na wenye visu vikali wakala nyama, mimi nikamwendea nikamwelezea kuwa anatakiwa ajitahidi kuwa mtulivu maana vijana wote mle ofisini tuna commitment zetu kwenye either ndoa ama mahusiano na wengine inasemekana wameathirika.Mimi akaniona eti mshamba natokea huko kwenye mkoa wa Operation Kimbunga.Sasa juzi kati kuna jamaa yupo njema ile mbaya akaniambia kuwa amepata mchumba na mchumba mwenyewe tupo kampuni moja kwa hiyo akawa ananiomba ushauri, nilivomuuliza akanitajia jina la bidada ambae kila siku nilikuwa namuambia atulizane.Yaani sikupepesa macho niliamuambia kila kitu kinachohusiana na huyo dada bila kuficha hata nukta.Jamaa kabwaga manayanga na wala sijutii moyoni ni sawa kabisa.Bottom line kwa wanaweke na wanaume tulizaneni na ndo zenu na kwa wakaka na wadada kama mnategemea kupata wenza waliotulia basi na nyi tulieni.

No comments:

Post a Comment

Adbox

@templatesyard