Katika eneo la tukio la mauaji hayo mlango wa nyumba ulikuwa umefungwa
kwa nje, na mara baada ya kufunguliwa maiti ya baba wa familia hiyo
Jonus Elias (44) ilikuwa sebuleni huku ikiwa imechinjwa, nako chumbani
kulikuwa na mwili wa mama wa familia hiyo Bi. Lucia Jonus na mwili wa
mtoto aliyekuwa na umri wa miezi saba.Polisi wakiondoa mwili wa marehemu Jones Lulinga, kutoka nyumbani kwake
kuupoeleka Hospitali baada ya kuuwa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu
wasiojukikana katika kijiji Ihila, Kata ya Buhingwa mkoa Mwanza jana Polisi akiwa ameubeba mwili wa mtoto aliyeuawa.Polisi wakishirikiana kupakia miili ya marehemu hao kwaajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi.Watu watatu wa familia moja wameuawa kikatili usiku wa kuamkia jana na
watu wanaosadikika kuwa ni majambazi katika kijiji cha Ihila B, Kata ya
Buhongwa Wilaya ya Nyamagana hapa Mkoani Mwanza.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kwamba watu hao ambao ni
Jonus Elius (44) ambae ni baba wa familia, Lucia Jonus (35) ambae ni
mama wa familia pamoja na Eliud Jonus (1) ambae ni mtoto wa familia hiyo
wameuawa kikatili kufuatia baba wa familia hiyo kuchinjwa shingoni na
kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali huku mama na mtoto wakisadikiwa
kunyongwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni waya.
Uchunguzi wa awali unaeleza kwamba kulikuwa na mgeni ambae alifika
katika familia hiyo ndani ya siku nne kwa ajili ya shughuli ya kufyatua
tofali za ujezi wa nyumba ya familia hiyo, ambae anasadikiwa kutenda
tukio hilo kwa kuwa baada ya mauaji hayo ametoweka katika familia hiyo.
Akiwa katika eneo la tukio Mkuu wa makosa ya upepelezi Mkoa wa Mwanza
RCO Joseph Konyo ameeleza kwamba mauaji hayo yanasadikika kutekelezwa
kati ya majira ya saa nane hadi saa kumi usiku wa kuamkia leo.
Aidha RCO Konyo amesema kwamba bado uchunguzi zaidi juu ya mauaji hayo
unaendelea na taarifa zaidi zitatolewa na msemaji wa jeshi la polisi
Mkoa wa wa Mwanza ambae ni RPC pindi upelelezi utakapokamilika ambapo
amewataka wananchi kutoa ushirikiano wao ili kuweza kufanikisha
upelelezi huo mapema.
Kufuatia mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yanasadikika kutekelezwa huku
sababu zikiwa bado ni kitendawili, wananchi na majirani wa eneo hilo la
tukio wameeleza kusikitishwa kwao na matukio ya aina hiyo ambayo
wametoa rai kwa jeshi la polisi kuhakikisha likamilisha upelelezi wake
mapema na kuhakikisha kwamba wahusika wote wanafikishwa katika vyombo
vya dola.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment