Mtoto Mitimo Clement(7)akitoa machozi baada ya kuzabuliwa makofi
kichwani na mjomba wake anayehafamika kwa jina la Dickson
Masabo(22)mbele ya askari Polisi katika Kituo Kipya cha mabasi mjini
Tabora eti kwa kudaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa akililia kusafiri na
shangazi yake.Bw.Dickson na mkewe wakifurahia kitendo cha kumpiga makofi mtoto huyo
mpaka kuanguka chini huku alama za vidole vya mkono wa Dickson vikibaki
kwenye upande wa uso wa mtoto huyo vikiashiria maumivu makali kutokana
na kipigo hicho kikali."Kwani vipi si nimempiga mimi ambaye ndiye ninamlea tatizo liko
wapi?"Dickson alisikika akiwajibu askari Polisi walioshudia tukio hilo.Baadhi ya askari Polisi wa Kituo cha mabasi Tabora mjini wakiwa na mtoto huyo huku Dickson naye akiwekwa chini ya ulinzi mkali.Dickson akiwa chini ya ulinzi wa Polisi kutokana na tukio hilo la kibabe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment