Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu,
mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi
wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai
walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .
Alisema kutokana fujo zilizofanywa na
baadhi ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa
nafasi yake angeweza kuagiza hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu,
lakini misingi ya dini yake haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha
unyenyekevu.
Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.
“Mimi ni mkristo, unyenyekevu ndiyo
nguzo pekee ya kuonyesha upendo na kudumisha amani. Ningeweza kuagiza
polisi wawadhibiti, lakini sioni sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya
utawala. Ndiyo maana nikaona bora nitumie njia nyingine ya kumshirikisha
Mungu mbele yao,”alisema Choya na kuongeza:
“Wanasiasa wamekuwa wakipandikiza chuki
kwa wananchi kwa makusudi kwa lengo la kuvuruga amani lakini kwa kumweka
Mungu mbele nina imani tutafanikiwa ili siku moja tusije tukaingia
kwenye mkumbo wa Syria na Misri”
Choya alitoa kauli hiyo jana alipokuwa
akizungumza na Mwananchi Jumapili, siku chache baada ya kitendo chake
cha kupiga magoti mbeye ya wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Haydom.
Mkuu huyo wa wilaya alidaiwa pia
kuwalaani baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Haydom kwa kile kinachodaiwa
kuwa ni kumdharau na kutofuata maagizo yake, wakati yeye amewasaidia
katika kutatua migogoro mbalimbali waliyokuwa nayo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza
baada ya wananchi wa kijiji hicho kupinga agizo la Choya, lililowataka
kufanya uchaguzi wa kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya
uchaguzi mdogo, ambapo walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.
Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu
huyo wa wilaya mbapo Choya alijibu; “Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin
akasema tena: “Unasema utarudi kwenu Biharamulo wakati hawakutaki kwani
ulifukuzwa ubunge?”
Maneno
hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku machozi
yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom kwani
wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba
msamaha mkuu huyo wa wilaya
No comments:
Post a Comment