Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young wa Philippines baada ya kutwaa taji hilo. Mrembo wa
Duinia 2013, Megan Young (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi wa
pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu
Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana. Warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo.
MREMBO
wa Philippines alivishwa taji la binti mzuri zaidi duniani mwaka huu
(2013) jana huko mjini Bali, Indonesia, ambapo kulikuwa na wasiwasi
kwamba Waislam wenye msimamo mkali walikuwa wamedhamiria kulivuruga
tukio hilo.
Mlimbwende
huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa Marekani,
ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji la
mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, na
akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi kutokea".
Maelfu
ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia mitaani tangu
mwezi uliopita wakipinga kufanyika kwa mashindano hayo nchini Indonesia,
nchi ambayo ina Waislam wengi zaidi duniani, wakiyaita mashindano hayo
kuwa ni “maonyesho ya ngono”.
Upinzani huo uliwalazimisha waandaji kulihamisha tukio hilo kutoka Jakarta kwenda Nusa Dua, kusini mwa Bali.
Katika
kulifahamu hilo mapema, balozi za Marekani, Uingereza na Australia
zilitoa vibali vya kwenda kwenye shindano hilo kwa kuwaonya wenye
kusafiri kwamba tukio hilo la mashindano ya urembo lilikuwa limepangwa
kuvurugwa. Hata hivyo, polisi wa Indonesia walisema hapakuwepo na vurugu
zozote siku ya Jumamosi.
Marine
Lorphelin, mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ufaransa, alishika nafasi ya
pili na Carranzar Naa Okailey Shooter (23) kutoka Ghana alikuwa wa tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment