Staa
wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa
atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza na mwanahabari
wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe ambaye ni memba wa kundi la muziki la
TNG alianika aya za Kurani kuwa katika Dini ya Kiislamu si ruhusa
kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito kwani ni sawa na kufunga
ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri ajifungue kwanza. “Ni kweli
mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua mapema mwezi
wanne, mwakani. “Kuhusu kufunga naye ndoa kwa sasa ni ngumu hadi
ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya hivyo lakini
atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema Malick. Malick ambaye hivi
sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema kuwa ana furaha kubwa
kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu Rose ajifungue salama
kwani anampenda kupita maelezo. Baada ya kuzungumza na Malick, gazeti
hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka, Batuli kufungukia ishu ya mwanaye
kubeba ujauzito kabla ya ndoa ambapo aligoma kuzungumza kwani
hakubaliani na suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment